
Meneja wa klabu ya Manchester City, Pep Guardiola anatarajiwa kuondoka klabuni hapo mwisho wa msimu wa 2025/26 wa Ligi kuu England baada ya mechi ya mwisho ya Ligi hiyo dhidi ya Aston Villa siku ya Jumapili akihitimisha utumishi wake wa muongo mmoja klabuni
Uamuzi uamuzi huo unaokuja masaa kadhaa baada ya kuiongoza klabu hiyo kutwaa ubingwa wa Kombe la FA kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Chelsea.
Kocha huyo wa zamani wa Barcelona mwenye umri wa miaka 55 alijiunga na klabu hiyo mnamo Juni 2016 akitokea Bayern Munich na kuiongoza klabu hiyo kutwaa makombe 20.
Man City inatarajiwa kutangaza kuondoka kwa Mhispania huyo siku ya Jumapili huku akitarajiwa kufanyiwa paredi la heshima kwenye mitaa ya Manchester siku ya Jumatatu.
