EWURA Yatangaza Bei Mpya za Mafuta, Petroli Yashuka Dar, Serikali Yaweka Ruzuku Kwenye Dizeli

EWURA Yatangaza Bei Mpya za Mafuta, Petroli Yashuka Dar, Serikali Yaweka Ruzuku Kwenye Dizeli
EWURA Yatangaza Bei Mpya za Mafuta, Petroli Yashuka Dar, Serikali Yaweka Ruzuku Kwenye Dizeli

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza rasmi bei mpya za kikomo za bidhaa za mafuta zitakazoanza kutumika nchini kuanzia leo Juni 3, 2026.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Gerald Maganga, bei ya petroli katika Jiji la Dar es Salaam imeshuka kwa shilingi 29 kwa lita, ambapo sasa itauzwa kwa shilingi 4,086 kutoka shilingi 4,115 iliyokuwa ikitumika mwezi Mei 2026.

Hata hivyo, kwa upande wa dizeli, bei imeongezeka kwa shilingi 85 kwa lita licha ya Serikali kuendelea kutoa ruzuku ya shilingi 534 kwa kila lita ya mafuta hayo.

Baada ya ruzuku hiyo, dizeli inayopitia Bandari ya Dar es Salaam sasa itauzwa kwa shilingi 4,333 kwa lita kutoka shilingi 4,248 ya mwezi uliopita.

EWURA imesema mabadiliko hayo yamechangiwa na mwenendo wa bei za mafuta katika soko la dunia, gharama za usafirishaji pamoja na mabadiliko ya thamani ya fedha za kigeni.

Mamlaka hiyo imewataka wauzaji wa mafuta nchini kuzingatia bei elekezi zilizotangazwa na kuhakikisha wanatoa risiti kwa wateja kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa.

Related Posts