
Ndoto ya kiungo wa Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’ ya kubeba Kiatu cha Mfungaji Bora wa Ligi Kuu ya Bara (2025/26) imezimika rasmi leo Juni 30, 2026.
Mshambuliaji wa Singida Black Stars, Mossi Ndumumwe, ameamua kufanya umafia wa soka kwa kupiga ‘Hat-trick’ safi kwenye mechi dhidi ya Fountain Gate na kufikisha mabao 17 msimu huu.
Msimamo ulivyokuwa kabla ya leo:
1️⃣ Fei Toto (Azam) – Mabao 15
2️⃣ Mossi Ndumumwe (Singida BS) – Mabao 14
3️⃣ Allan Okello (Yanga) – Mabao 14
Kwa soka hili la leo, Mossi amewafunika Fei Toto na Allan Okello na kuondoka na tuzo kibindoni. Pole sana kwa Fei Toto aliyeweka pambano kubwa msimu mzima!
