
Simba SC imekamilisha usajili wa mshambuliaji Ismail Mgunda kutoka Mashujaa FC kwa mkataba wa miaka miwili, leo Agosti 15, 2026.
Mshambuliaji huyo wa Kitanzania mwenye umri wa miaka 31 anatarajiwa kuongeza chachu na ushindani wa namba kwenye safu ya ushambuliaji ya Wekundu wa Msimbazi, wakati huu klabu ikiendelea kusuka kikosi cha ushindani kwa ajili ya msimu wa 2026/27.
Ujio wa Mgunda unampa wigo mpana kocha na benchi la ufundi la Simba katika kupanga kikosi kitakachowania mataji ya ndani na kuwakilisha vyema nchi kwenye michuano ya kimataifa.
Karibu Msimbazi, Ismail Mgunda!
