
Klabu ya Singida Black Stars imemtambulisha rasmi winga Ladack Chasambi kama mchezaji mpya klabuni hapo, ikimsajili kwa uhamisho huru baada ya kuachana na waliokuwa waajiri wake, Simba SC.
Chasambi 22, raia wa Tanzania anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha Singida Black Stars kwa ajili ya msimu ujao wa mashindano wa 2026/27.
