Ngorongoro Heroes Yatinga Fainali AFCON U20 CECAFA Kwa Kuichapa Burundi 2-0

Timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes, imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya mashindano ya kuwania kufuzu Kombe la Mataifa Afrika (AFCON U20) kwa ukanda wa CECAFA baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 2-0 dhidi ya Burundi katika mchezo wa nusu fainali.

Katika mchezo huo uliokuwa wa vuta ni kuvute, Ngorongoro Heroes walianza kwa kasi na kupata bao la kuongoza mapema mnamo dakika ya 17 kupitia kwa Juma Abushiri. Vijana hao walizidi kuliandama lango la Burundi na kufanikiwa kupata bao la pili dakika ya 33 kupitia kwa Faraji Kayanda, bao lililoweka amani na kuhakikisha Tanzania inaenda mapumziko ikiwa kifua mbele.

Kipindi cha pili kilishuhudia safu ya ulinzi ya Tanzania ikisimama imara na kulinda ushindi huo hadi filimbi ya mwisho.

Matokeo ya Mchezo (FT):

  • Tanzania U20 🇹🇿 2-0 🇧🇮 Burundi U20

  • âš½ 17’ Juma Abushiri

  • âš½ 33’ Faraji Kayanda

Kwa ushindi huu, Ngorongoro Heroes haijatinga fainali tu, bali pia imekata tiketi ya kushiriki fainali kuu za Kombe la Mataifa Afrika kwa vijana (AFCON U20).

Related Posts