Yanga Yawasba Moto Sokoni: Yawatambulisha Touré, Zakouani na Kangwanda

Yanga Yawasba Moto Sokoni: Yawatambulisha Touré, Zakouani na Kangwanda
Yanga Yawasba Moto Sokoni: Yawatambulisha Touré, Zakouani na Kangwanda

Yanga Yawasba Moto Sokoni: Yawatambulisha Touré, Zakouani na Kangwanda

Young Africans SC imeendelea kuonyesha umakini wake katika kuimarisha kikosi kuelekea msimu wa 2026/27 baada ya kuwatambulisha rasmi wachezaji watatu wapya wenye uzoefu wa kimataifa.

Usajili huu mpya unalenga kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji na ubawa, huku klabu hiyo ikipania kufanya vizuri katika Ligi Kuu ya NBC, Kombe la Shirikisho la CRDB, na mashindano ya CAF.

Wachezaji Wapya na Profile Zao:

  • Cheikh Ibrahima Touré (29) – Mshambuliaji Mfaransa huyo aliyejiunga akitokea Al-Jabalain FC ya Saudi Arabia ana uwezo wa kucheza kama mshambuliaji wa kati (namba 9) au kutokea pembeni. Katika msimu wa 2025/26, Touré alikuwa nguzo muhimu katika Ligi Daraja la Kwanza nchini Saudi Arabia, akisifiwa kwa nguvu, kasi, na umahiri wa kupachika mabao.

  • Housseine Zakouani (28) – Winga Mchezaji huyu wa Timu ya Taifa ya Comoro amejiunga na Yanga akitokea Al-Zulfi FC ya Saudi Arabia. Zakouani anajulikana kwa kasi, uwezo wa kutengeneza nafasi, na kufunga mabao, sifa zilizomfanya kuwa mchezaji tegemeo kitaifa na klabuni.

  • Albert Kangwanda (27) – Winga wa Kushoto Akitokea Red Arrows FC ya Zambia, Kangwanda ni mchezaji mwingine wa kimataifa anayeingia kikosini. Akiwa mchezaji wa Timu ya Taifa ya Zambia, ameonyesha ubora mkubwa katika Ligi Kuu ya Zambia na mashindano ya CAF kupitia chenga, kasi, na pasi zake za mabao kutoka upande wa kushoto.

Usajili wa nyota hawa watatu unaashiria madhamira ya Wananchi kuendelea kutawala soka la ndani na kufika mbali zaidi barani Afrika msimu ujao.

Related Posts