Sakata la Simba na Wydad Kuhusu Mchezaji Seleman Mwalimu Bado Kizungumkuti

 

Makubaliano kati ya Simba na Wydad Athletic Club ni uhamisho wa mkopo wa msimu mzima wa 2026/27 wa Mchezaji Seleman Mwalimu ambapo Uongozi wa Wydad chini ya Rais Hicham Ait Menna ulikubali kuwa Simba wanapaswa kuingiza dola 50,000 za Kimarekani mwishoni mwa mwezi huu Julai.

Utata unatoka wapi? Ni baada ya Uongozi mpya uliochaguliwa chini ya Rais Ibrahim El Asri ambaye hawatambui suala hilo ikionekana changamoto ni kwenye kukabidhiana ofisi kati ya Uongozi wa mwanzo na wa sasa ambapo Uongozi mpya umeingia madarakani hapo jana.

Simba wanasema Emails zote za makubaliano kati yao na Wydad wanazo na watarejea emails hizo na makubaliano yao endapo Uongozi wa sasa utaridhia basi Gomez atasalia Msimbazi ila kama watakataa basi Gomez atarudi nchini Morocco 🇲🇦 ila mchakato uliopo ni kurejea Emails za makubaliano.

Related Posts