
Nyota wa timu ya Taifa ya Tanzania, Adolf Mtasingwa Bitegeko amecheza dakika zote 90 wakati timu yake ya Kaizer Chiefs ikishinda taji la Toyota Cup 2026 kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Mabingwa wa Ligi kuu Zimbabwe, Scottland FC.
Kaizer Chiefs imetwaa Kombe hilo kwa mara kwa kwanza baada ya misimu mitatu tangu Kombe hilo lilipoanzishwa mwaka 2024 kwa ushirikiano kati ya klabu hiyo na kampuni ya Toyota South Africa Motors, ikipigika 4-0 dhidi ya Yanga SC mwaka 2024 na Asante Kotoko kwa penalti 3-1 mwaka 2025
FT: Kaizer Chiefs 🇿🇦 1-0 🇿🇼 Scottland FC
15’ Mfundo Vilakazi
