KIMENUKA: Timu za Ulaya Zafikiria Kususia Kombe la Dunia 2030

KIMENUKA: Timu za Ulaya Zafikiria Kususia Kombe la Dunia 2030
KIMENUKA: Timu za Ulaya Zafikiria Kususia Kombe la Dunia 2030

UEFA, chombo kinachosimamia soka barani Ulaya, kinatafakari uwezekano wa kususia matukio yajayo ya FIFA, ikiwemo Kombe la Dunia saa chache baada ya Shirikisho hilo kuelezea ghadhabu yake kuhusu mipango ya FIFA ya kuuza hisa za wachache katika mashindano hayo kwa wawekezaji binafsi.

Katika makubaliano FIFA inapanga kuchangisha kiasi kinachokadiriwa kuwa Dola Bilioni 4.2 mwaka wa 2026 kwa kuuza hisa asilimia 20 katika Kampuni tanzu mpya.

FIFA ilithibitisha mipango hiyo katika taarifa, ikieleza kuwa Kampuni hiyo mpya itaitwa FIFA Forward Enterprise na itasimamia shughuli za kibiashara na za matukio ya Shirikisho hilo.

Shirikisho hilo lilisema kuwa vyama 211 wanachama wa FIFA kila kimoja kingepokea ufadhili wa Dola Milion 20 iwapo makubaliano hayo yatafanikiwa, na kwamba fedha zinazotolewa kwa Wanachama kila mwaka zingeendelea kuongezeka hadi mwaka wa 2038.

Related Posts