
EXCLUSIVELY: Wydad AC Yamwagia Yanga Bilioni 1.9TSh Kumtaka Allan Okello, Aziz Ki Ametajwa Mbadala Wake
DAR ES SALAAM β Klabu ya Young Africans SC imepokea ofa mnono ya dola za Kimarekani USD 750,000 (sawa na takribani Shilingi Biliioni 1.9 za Kitanzania) kutoka kwa miamba ya Morocco, Wydad Athletic Club (Wydad AC), wakihitaji saini ya kiungo mshambuliaji raia wa Uganda, Allan Okello (25), kuelekea msimu wa 2026/27.
Taarifa za ndani zinaeleza kuwa Uongozi wa Yanga umeijibu Wydad AC kuwa utatoa msimamo rasmi mara baada ya kukamilika kwa mchezo wa Dabi ya Kariakoo.
Lengo kuu la Yanga kusubiri ni kutathmini iwapo fedha hizo zitatumika kukamilisha mchakato wa kumrejesha klabuni hapo kiungo wao wa zamani, Stephane Aziz Ki, ambaye kwa sasa anaipiga kunako klabu ya Al Ittihad SC ya nchini Libya.
