Yanga SC Yamtambulisha Rasmi Stephane Aziz Ki: Rejea Mfalme wa Jangwani

Klabu ya Yanga SC imehitimisha uvumi wa muda mrefu baada ya kumtambulisha rasmi kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Burkina Faso, Stephane Aziz Ki, ambaye anarejea klabuni hapo baada ya kuondoka mwaka 2025.

Aziz Ki, ambaye aliondoka Jangwani na kujiunga na Wydad Casablanca ya Morocco kabla ya kutimkia Al-Ittihad Tripoli ya Libya, anarudi nyumbani akiwa na kumbukumbu za mafanikio makubwa aliyoyapata akiwa na Wananchi.

Urejeo wa nyota huyo unatajwa kuwa chachu kubwa ya kuongeza ufanisi na ubunifu katika safu ya kiungo mshambuliaji kuelekea kampeni za msimu wa 2026/27, huku benchi la ufundi likipata chaguo la ziada na la kiwango cha juu duniani.

Mashabiki wa Yanga SC wameupokea usajili huo kwa msisimko mkubwa, wakiamini uwepo wake utaendeleza utawala wa timu hiyo katika soka la ndani na kimataifa.

Related Posts