
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 25 Agosti, 2026, amepokea barua ya ombi la kujiuzulu Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi kuanzia tarehe 04 Septemba, 2026.
Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka imeeleza yafuatayo “Mheshimiwa Rais ameridhia ombi hilo, taratibu za Kikatiba za kumpata Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwingine zitachukuliwa”
