
TFF Yamfungia Jamal Bakhresa Kujishughulisha na Mpira Kwa Mwaka Mmoja
Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemfungia Kiongozi wa Azam FC, Jamal Bakhresa, kujishughulisha na mpira wa miguu kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Bakhresa ametiwa hatiani kutokana na vitendo vya utovu wa nidhamu alivyofanya kabla na baada ya mechi ya Fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB iliyochezwa kisiwani Pemba. Mlalamikiwa alikiri kufanya makosa mbele ya Kamati hiyo inayoongozwa na Wakili Alex Mushumbusi, na kuomba radhi kwa TFF kwa makosa aliyoyafanya.
Kamati ilimtia hatiani kwa kuzingatia Ibara ya 11(f) ya Kanuni za Nidhamu za TFF, Toleo la 2021, huku akiahidi kutotorudia tena vitendo hivyo. Taarifa hiyo imetolewa leo, Agosti 22, 2026, na Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Clifford Mario Ndimbo.
