
Watanzania 300 wanatarajiwa kuwasili leo Nchini Tanzania wakitokea Afrika Kusini, kufuatia operesheni ya kuwaondoa Raia wa kigeni waliopo Nchini humo.
Leo Septemba 3, 2026, katika Ukumbi wa Woodstock Town Hall Jijini Cape Town, Afrika Kusini, limefanyika zoezi la kuwaandaa Watanzania hao kwa ajili ya safari ya kurejea Nchini.
Kwa mujibu wa Balozi wa Tanzania Nchini Afrika Kusini, James Bwana, hadi kufikia jana (Septemba 02,2026) Watanzania 200 walikuwa wamejiandikisha kwa ajili ya safari hiyo, lakini idadi imeongezeka na kufikia 300 wakati maandalizi ya safari yakianza.
Watanzania hao wanarejea Tanzania kwa msaada wa usafiri ulioandaliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya kutoa ridhaa yao ya kurejea kwa hiari.
