
VIDEO; Nyumba ya Mwijaku Yaungua Moto, Afunguka Kunusurika
Nyumba ya mtangazaji na mfanyabiashara mashuhuri nchini, Mwijaku, imenusurika kuteketea kwa moto kufuatia hatua za haraka na za awali kuchukuliwa na kufanikiwa kudhibiti moto huo kabla ya kusababisha madhara makubwa.
Kupitia video aliyoiweka kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, Mwijaku ameonekana mwenye furaha na amani huku akimshukuru Mungu kwa kumnusuru na janga hilo kubwa la moto. Mtangazaji huyo amewatoa hofu mashabiki na wafuasi wake kwa kueleza kuwa mali zake zote ziko salama na hakuna madhara yoyote makubwa yaliyotokea.
Tukio hilo limeacha hisia za shukrani kubwa kwa Mwijaku na familia yake, kwani udhibiti wa haraka na kwa wakati wa moto huo umezuia maafa yaliyoweza kutokea na kuokoa jumba lake pamoja na mali zilizomo ndani.
TAZAMA VIDEO
View this post on Instagram
