Rais Samia Ateua Viongozi Wapya, Amtengua RC Tabora

Rais Samia Ateua Viongozi Wapya, Amtengua RC Tabora
Rais Samia Ateua Viongozi Wapya, Amtengua RC Tabora

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi wapya ambapo amemteua Bi. Angeline Lubala Mabula kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, akichukua nafasi ya Bw. Beno Morris Malisa ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Kwa mujibu wa taarifa leo Oktoba 28, 2026 iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka
Rais Samia pia amemteua Dunford George Mpelumbe kuwa Mwenyekiti mpya wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) ambapo kabla ya uteuzi huo, Mpelumbe alikuwa Wakili wa Serikali katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, na sasa anachukua nafasi ya Jaji Mstaafu Mathew Pauwa Mwaimu ambaye amemaliza muda wake wa utumishi.

Rais pia amemteua Omar Ali Omar kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo ya Haki za Binadamu na Utawala Bora akichukua nafasi ya Mohamed Khamis Hamad ambaye amehitimisha muda wake wa utumishi. Kabla ya uteuzi huo, Omar alikuwa Mkuu wa Idara ya Utawala, Mipango na Fedha katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume, Zanzibar.

Taarifa hiyo iliyosainiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais (Ikulu), Shaaban Kissu, imebainisha kuwa uapisho wa viongozi hawa wateule utafanyika kwa tarehe itakayopangwa baadaye.

Related Posts