Padri Kitima Afunguka: Taifa Litubu, Tubadilike

Padri Kitima Afunguka: Taifa Litubu, Tubadilike
Padri Kitima Afunguka: Taifa Litubu, Tubadilike

Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima, amewataka Watanzania kutubu dhambi za kiburi na kuacha matendo maovu ili kupata msamaha wa kweli na kudumisha amani ya Taifa.

Padri Kitima ametoa wito huo leo, Oktoba 29, 2026, Kanisani wakati wa Misa ya kuwaombea Marehemu na Waathirika wa matukio ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, akisisitiza umuhimu wa kuondoa kiburi katika masuala ya kisiasa na kutubu dhambi.

“Tujifunze kwa matukio yale, kama Taifa tukiendekeza uovu na kiburi tutaangamia, tujifunze katika hilo, hatuna budi kama Taifa kutubu, Tanzania ni kisiwa cha amani, kimbilio la Wakimbizi na ni Kituo cha Elimu ya kujikomboa na ndiyo Taifa la kuwaletea wengine uhuru, tutubu, tubadilike,” amesema Padri Kitima.

Related Posts