
Kwa taarifa za ndani na za uhakika kabisa kutoka makao makuu ya klabu, “Mwamba” ndiye kocha mpya wa Yanga SC baada ya mchujo mkali uliovuta hisa za wengi!
Kama unakumbuka, Sead Ramovic aliwahi kupita Yanga kwa muda mfupi na kujipatia nafasi kubwa mioyoni mwa Wanayanga kutokana na staili yake ya kusisimua ya soka la “Gusa Achia Twende”.
Haya sasa Wananchi, falsafa ile inayopendwa na wengi imerudi rasmi pale Jangwani! Je, uamuzi huu utaleta tija gani kikosini? Weka maoni yako hapa chini!
