Nature

Jeshi la Rwanda Limekanusha Taarifa Zinazodai Kuwa Afya ya Rais Paul Kagame iko Hatarini Sana

Jeshi la Rwanda limekanusha vikali taarifa zinazodai kuwa afya ya Rais Paul Kagame iko “hatarini sana”, likiitaja habari hiyo kuwa ni ya uongo na yenye nia ya kupotosha umma.

Taarifa hizo zimeibuka baada ya Rais Kagame kutoonekana hadharani kwa takriban wiki tatu, hali ambayo imeibua mjadala mkali kwenye mitandao ya kijamii na majukwaa ya kisiasa. Hali hiyo imetumiwa na baadhi ya wapinzani wake kueneza madai kuhusu afya yake.

Miongoni mwa waliodai hayo ni David Himbara, mpinzani wa serikali ya Kigali anayeishi uhamishoni na aliyewahi kuwa mshauri wa masuala ya uchumi wa Kagame, ambaye amedai kuwa Rais huyo yuko Ujerumani kwa matibabu.

Hata hivyo, msemaji wa serikali ya Rwanda, Yolande Makolo, alinukuliwa na gazeti la Taarifa akieleza kuwa Rais Kagame yuko salama na anapumzika kama binadamu mwingine yeyote: “Rais yuko vizuri na anapumzika kawaida,” alisema Makolo.

Kwa mujibu wa rekodi rasmi, Rais Kagame alionekana hadharani kwa mara ya mwisho tarehe 6 Juni 2025, alipokutana na kikundi kutoka shule ya Hope Haven Christian School jijini Kigali.

Shirika la habari la Uingereza BBC, limeripoti kuwa juhudi zake za kuwasiliana na ofisi ya Rais kuhusu madai haya hazijazaa matunda hadi sasa. Hata hivyo, jeshi la Rwanda limesisitiza kuwa taarifa kuhusu afya ya Rais ni za uongo na linazitaka taasisi na watu binafsi kuwa makini na uzushi usio na msingi wowote

Related Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *