
Jeshi la Polisi la Polisi Tanzania limesema limeziona taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu Humphrey Polepole kutekwa na tayari limeanza kufanyia kazi taarifa husika ili
kupata ukweli wake.
Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi Makao Makuu ya Polisi Dodoma, leo October 06,2025 imenukuliwa ikieleza yafuatayo “Jeshi la Polisi lingependa kutoa taarifa kuwa bado linaendelea kumsubiri Ndg. Humphrey Polepole aripoti katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, alitumiwa barua ya wito kwa mujibu wa sheria za Nchi aripoti katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai ili atoe maelezo kuhusiana na tuhuma mbalimbali alizozitoa kupitia Mitandao ya Kijamii lakini hadi leo hajatekeleza maelekezo hayo kwa mujibu wa sheria”
“Jeshi la Polisi limeona taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na Ndugu zake kuwa ametekwa, tayari tumeanza kufanyia kazi taarifa husika ili kupata ukweli wake” ——— imeeleza taarifa ya Jeshi la Polisi.

