Nature

BREAKING; Rais Samia Amteua Mwigulu Nchemba Kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania

Breaking News:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Mwigulu Nchemba kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa mjibu wa Hati iliyowasilishwa leo Bungeni Jijini Dodoma Novemba 13, 2025, na Mpambe na Mshauri Masuala ya Kijeshi wa Rais, Brigedia Jenerali Nyamburi Mashauri ikiwa ndani ya bahasha kisha kufunguliwa na Spika wa Bunge Mhe. Mussa Azzan Zungu ambaye amewasomea wabunge na kutaja jina la Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi na aliyekuwa Waziri wa Fedha katika awamu iliyopita

Baada ya hapo wabunge watampigia kura kumthibitisha Waziri Mkuu aliyependekezwa kwa Azimio litakalopitishwa na Bunge.

Related Posts