Mchezaji Khalid Aucho Aingizwa Kwenye Dili la Okello Yanga

Uongozi wa Yanga SC umempa jukumu maalum aliyekuwa kiungo na nahodha wa timu ya taifa ya Uganda, Khalid Aucho, kumshawishi nyota mwenzake wa Uganda, Allan Okello, kujiunga na klabu hiyo ya Jangwani.

Kwa mujibu wa taarifa, Yanga inaona uwepo wa Aucho kama daraja muhimu kutokana na uhusiano wake mzuri na Okello pamoja na uzoefu wake mkubwa ndani na nje ya uwanja, jambo linaloweza kusaidia kufanikisha dili hilo.

Allan Okello, anayesifika kwa ubunifu, uwezo wa kutengeneza nafasi na kufumania nyavu, anatajwa kuwa mmoja wa wachezaji wanaofuatiliwa kwa karibu na Rais wa Yanga katika mipango ya kuimarisha safu ya kiungo mshambuliaji.

Hatua ya Yanga kumtumia Aucho inaonyesha dhamira ya dhati ya klabu hiyo katika kumsajili Okello, huku mashabiki wakisubiri kuona kama ushawishi huo utafanikiwa kumleta nyota huyo Jangwani.

Related Posts