Clemence Mwandambo Anashikiliwa na Polisi Mbeya..Kisa Hichi Hapa

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Mwalimu wa Shule ya Awali Saint Clemence, Clemence Kenani Mwandambo, mkazi wa Uzunguni “A” jijini Mbeya, kwa tuhuma za kuchapisha na kusambaza taarifa za uongo pamoja na kukashifu imani za dini mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Desemba 29, 2025 na Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, mtuhumiwa alikamatwa alfajiri majira ya saa 10:00 katika maeneo ya Uzunguni.

Kwa mjibu wa Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, SACP Benjamin Kuzaga imeeleza kuwa Mwandambo alikuwa akitumia akaunti zake za mitandao kusambaza ujumbe unaodaiwa kupotosha na wenye kuleta mgawanyiko wa kiimani.

Jeshi la Polisi limesema uchunguzi unaendelea ili kukamilisha hatua zinazofuata za kisheria, endapo ushahidi utathibitisha tuhuma zinazomkabili.

Related Posts