Ally Mayai Atajwa Kutangaza Nia ya Kugombea Urais TFF
Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) unaotarajiwa kufanyika tarehe 16 Agosti 2025 mkoani Tanga, hekaheka za kisiasa ndani ya soka zimeanza kushika kasi huku majina ya watu maarufu katika uongozi wa mpira yakianza kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali.
Uchaguzi huo mkubwa utahusisha nafasi ya Urais wa TFF (nafasi moja) pamoja na wajumbe wa Kamati ya Utendaji (nafasi sita), ambapo tayari baadhi ya wadau wa soka wameonyesha nia ya kuchukua fomu za kuwania nafasi hizo muhimu katika uendeshaji wa soka nchini.
Miongoni mwa waliotajwa kuwa na nia ya kugombea nafasi ya Urais ni Ally Mayai, ambaye si mgeni kwenye medani ya siasa za soka Tanzania. Mayai amekuwa akihusishwa mara kadhaa na nia ya kuliongoza shirikisho hilo, ikiwa ni pamoja na kujaribu kugombea kwenye uchaguzi uliopita, ambapo hata hivyo alikosa sifa za kisheria, na hivyo kumwacha mgombea pekee Wallace Karia, ambaye alishinda kwa kishindo bila kupingwa.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka TFF, mchakato wa uchukuaji wa fomu za kugombea utaanza rasmi leo, Jumapili ya tarehe 16 Juni hadi tarehe 20 Juni 2025, ambapo wagombea watapewa nafasi ya kuchukua fomu, kujaza taarifa muhimu na kurudisha kwa mujibu wa kanuni na taratibu zilizowekwa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF.
Wadadisi wa mambo ya soka wanasema kuwa uchaguzi huu utakuwa wa aina yake kutokana na matarajio makubwa ya mabadiliko kutoka kwa wadau mbalimbali wa soka nchini, huku kukiwa na shinikizo la kuongeza uwajibikaji, uwazi na maendeleo ya kweli katika sekta ya mpira wa miguu.
Endapo Ally Mayai atakidhi vigezo safari hii, atakuwa miongoni mwa wagombea watakaomkabili Wallace Karia endapo naye atatangaza nia ya kutetea kiti chake kwa awamu nyingine. Hii ni fursa ya pili kwa Mayai, na huenda safari hii akaibuka na mafanikio zaidi ya uchaguzi uliopita.
Kwa sasa macho ya mashabiki wa soka, wadau wa michezo, na wanahabari yameelekezwa Tanga, ambako historia mpya ya uongozi wa mpira nchini Tanzania inatarajiwa kuandikwa Agosti mwaka huu.
ALSO READ | Mangungu Awaonya Wanaotaka Kuchukua Nafasi ya Karia Urais TFF
Alikataa kuolewa ili amkomboe mama yake... Lakini mama ndiye aliyemuuza!
GORYANAH –Hii ni story ya Moto Sana yenye hisia na Mafunzo, binti jasiri anayepambana na siri nzito, umaskini na hatari kubwa kwa ndoto zake! Pakua app yetu ufurahie Sehemu ya 1 Hadi ya 5,na mwendelezo wake kila JUMAMOSI SAA MOJA KAMILI JIONI BURE!
Ukiona ujumbe wa allow notification bonyeza allow ili uwe mwanafamilia.