
Mchambuzi wa soka Edo Kumwembe amehoji kwanini baadhi ya Watanzania wanashangilia baada ya Hassan Mwakinyo kupoteza pambano lake dhidi ya Michael Soro wa Ivory Coast.
“Hiki kitu kimeniuma, lakini sina cha kufanya. Watanzania wengi wanashangilia mjomba wangu, Hassan Mwakinyo Jr, kupoteza pambano lake. Nimemuita mjomba kwa sababu mama yangu anatokea Tanga.”
“Tatizo ni mjomba Hassan au Watanzania? Tufungue mjadala. Ingekuwa ni pambano la ndani, isingekuwa shida. Lakini sisi na yule jamaa Soro, ilipaswa kuwa ni pambano la SISI dhidi ya YEYE.”
“Hili limekuwa tofauti. Imekuwa kama vile SISI na Soro dhidi ya Mjomba Hassan. Labda kuna mahali Anko amekosea wakati akijenga maisha yake katika mchezo huu.”
“Vyovyote ilivyo, yeye ndiye bondia bora zaidi Tanzania kwa sasa. Hata hivyo, kuwa na mahusiano mazuri na jamii yako ni jambo muhimu katika maisha ya kila siku.”
“Nani anamchukia Mbwana Samatta kiasi cha kufurahia akikosa goli? Sidhani. All the best, Anko Hassan. We will rise again…” – Edo Kumwembe.
