Kocha wa timu ya taifa ya Burkina Faso, Brama Traore amemjumuisha tena Stepane Aziz Ki katika kikosi cha taifa hilo kitakachoingia kambini kujiandaa na mechi za kuwania kufuzu kombe la dunia dhidi ya Tunisia na Zimbabwe zitakazopigwa mapema mwezi Juni.

Chama cha soka cha Burkina Faso ‘FBF’ kimemtambua Stephane Aziz ki kama mchezaji wa klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco na si Yanga SC.

Ikumbukwe Yanga SC kupitia ofisa habari wake Ally Kamwe alisema Aziz Ki bado ni mchezaji halali wa vinara hao wa ligi kuu huku akiweka wazi bado hawajamalizana na klabu inayomtaka mchezaji huyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *