JamiiCheck imefuatilia Uhalisia wa Picha za Boniface Mwangi zilizosambazwa Mtandaoni zikimuonesha akiwa na majeraha zikidaiwa kuwa ni za tukio la Mei 22, 2025 na kubaini kuwa ni Upotoshaji.
–
Kwa kutumia nyenzo ya Kimtandao ya #TinEye, JamiiCheck imejiridhisha kuwa picha hizo zilichapishwa na Mwangi Aprili 21, 2025 katika mtandao wake wa X akielezea tukio la kushambuliwa kwake na aliowataja kuwa ni Polisi wa Nairobi.
