Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu ya Yanga Sc ametoa ufafanuzi kuhusu mkataba wa kiungo Stephanie Aziz Ki na klabu ya Wydad Casablanca na kueleza kuwa makubaliano yao ilikuwa ni kuwatumikia Wydad kwa mkataba wa miezi mitatu.

Kamwe amebainisha kwamba mkataba huo una vipengele viwili ambapo ikiwa miamba hiyo ya Morocco itaridhishwa na kiwango chake basi watamuongezea mkataba wa miaka miwili na ikiwa vinginevyo basi atarejea Jangwani na atakuwepo kwenye mchezo wa Ngao ya Jami..

“Kwa mujibu wa makubaliano ilikuwa hadi kufikia Julai 10 Wydad wawe wameshawasiliana na Yanga Sc. Kama Wydad watakuwa wanaongeza maana yake wamalizie kiasi ambacho tulikubaliana ila kama watasema arudi sawa arudi aje awashone maana bado amebaki na mwaka mmoja.”——amesema Kamwe.

Katika hatua nyingine, Kamwe ameweka wazi kuwa tayari kocha mpya ameshatua klabuni hapo na kwa sasa anapitia ‘mafaili’ ya watangulizi wake kabla ya kutambulishwa rasmi na kuanza mchakato wa usajili.


Alikataa kuolewa ili amkomboe mama yake... Lakini mama ndiye aliyemuuza!

GORYANAH –Hii ni story ya Moto Sana yenye hisia na Mafunzo, binti jasiri anayepambana na siri nzito, umaskini na hatari kubwa kwa ndoto zake! Pakua app yetu ufurahie Sehemu ya 1 Hadi ya 5,na mwendelezo wake kila JUMAMOSI SAA MOJA KAMILI JIONI BURE!

BONYEZA HAPA KU DOWNLOAD.

Ukiona ujumbe wa allow notification bonyeza allow ili uwe mwanafamilia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *