
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limemfungia Halima Haji wa Kibaokata kutojishughulisha na sanaa kwa miaka mitatu kwa kosa la kusambaza video isiyozingatia maadili.
Aidha, BASATA imemtaka msanii huyo kulipa faini TZS milioni 3 ndani ya siku 14 tangu kutolewa kwa adhabu hiyo, pamoja na kuondoa kipande cha video hiyo kwenye mitandao ya kijamii.
