Mbunge wa Viti Maalum Halima Idd Nassor (46) amefariki dunia leo Januari 18, 2026 akipatiwa matibabu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.
Taarifa ya kifo chake imetolewa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Azzan Zungu ikisema “Kwa masikitiko makubwa, natangaza kifo cha Mbunge wa Viti Mheshimiwa Halima Idd Nassoro kilichotokea leo 18 Januari, 2026 Jijini Dar es Salaam. Natoa pole kwa Waheshimiwa Wabunge wote, familia ya Marehemu, ndugu, jamaa na marafiki, Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu,”
Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa mipango ya mazishi inaendelea kufanyika kwa ushirikiano wa bunge na familia ya Halima.
