Chadema Yaitisha Kikao Kamati Kuu Mei 21
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinatarajia kufanya kikao cha Kamati Kuu, Mei 21, 2025, jijini Dar es Salaam ambapo ‘No reform no election’ inatajwa kuwa miongoni mwa ajenda zitakazojadiliwa.
Kikao hicho kimeitishwa na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA (Bara), John Heche, ambaye amesema ajenda kuu zitakuwa kujadili masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kampeni ya “No Reforms, No Election” (Bila mabadiliko Hakuna Uchaguzi).