
Yanga ushindi wao unaanza kwanza kwenye spirit yao ya kutaka ushindi kivyovyote — kila mtu anavuja jasho ipasavyo.
Kuna muda Boka alipiga pasi mbovu, Diarra nusu amtwange ngumi hapo ni wakati timu inaongoza mbili bila.
Angalia Yao na ile njaa yake ya kulazimisha Yanga ishambulie muda wote. Yupo juu muda wote kama winga.
Muangalie Max anavyohangaika kulia na kushoto, juu na chini, ili tu afunge bao.
Mchungulie Dube pale juu, timu inaongoza mbili lakini bado unamkuta offside mara tatu na analalamika kabisa.
Hii hali pamoja na ubora wao ndiyo inawapa performance yao back to back. Jamani huu ni mwaka wa tano timu hii inakaribia ubingwa mfululizo 🙌🙌
✍️KALAMU YA USHAHIDI
@cheyolutenganotz
