Feisal Salum Mchezaji Anaewaaminisha Wachezaji Wazawa Kuwa Wanaweza Mbele ya Wageni….
KIUNGO mshambuliaji wa matajiri wa Jiji la Dar es Salaam Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’, ndiye mchezaji aliyechangia mabao mengi zaidi (27) katika Ligi Kuu Bara kwa mwaka 2024 (Januari 1 hadi Disemba 31,), baada ya kufunga 15 na kuasisti 12.
.
Kiwango bora cha Feisal kilimfanya kumaliza na mabao 19 ya Ligi Kuu Bara kwa msimu uliopita, akiwa ndiye mchezaji mzawa aliyeshika nafasi ya kwanza kwa waliofunga mabao mengi zaidi, akizidiwa tu na Stephane Aziz KI wa Yanga aliyefunga 21.