Geita Gold Yapigwa Faini ya 10 Milion Kwa Kukiuka Taratibu za Ligi

Geita Gold Yapigwa Faini ya 10 Milion Kwa Kukiuka Taratibu za Ligi
Geita Gold Yapigwa Faini ya 10 Milion Kwa Kukiuka Taratibu za Ligi

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Septemba 3, 2026 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya maamuzi yafuatayo;

Klabu ya Geita Gold imepewa Onyo kali kwa kosa la maafisa wake kuchelewa kwa dakika 15 kufika kwenye kikao cha kitaalamu cha maandalizi na uratibu wa mchezo.

Adhabu hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 17:62 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

Aidha Klabu hiyo pia imetozwa faini ya Sh.10,000,000 (milioni kumi) kwa kosa la kuwakilishwa na maafisa wawili pekee kwenye kikao cha kitaalamu cha maandalizi na uratibu wa mchezo kinyume na matakwa ya kanuni ya 17.29(2.1.1).

Adhabu hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 17:62 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

Related Posts