Kipa wa zamani wa timu ya Taifa Tanzania @taifastars_ na Yanga SC, Peter Manyika amefariki dunia Alfajiri ya leo katika Hospital ya St. Monica, DSM.
Mwili wake umepelekwa kuhifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala huku chanzo cha kifo chake kikielezwa kuwa ni kuugua kwa muda mrefu.
