
Mwanamitindo maarufu Hamisa Mobetto na mwigizaji Zaiylissa wameibua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki baada ya kuwasili katika hafla iliyofanyika ndani ya Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Wawili hao waliiba macho ya wengi baada ya kuwasili katika hafla iliyofanyika ndani ya Mlimani City, jijini Dar es Salaam, akiwa katika muonekano wa kuvutia na wa kifahari.
Muonekano wao uliibua mijadala mikubwa mitandaoni, ambapo mashabiki waligawanyika kuhusu nani aling’ara zaidi katika usiku huo maalum.
Mwanamitindo na mwigizaji Zaiylissa
Baadhi ya mashabiki walimsifu Hamisa Mobetto kwa mwonekano wake wa kifahari, kujiamini na namna alivyoendana na tukio hilo. Wengine walieleza kuvutiwa zaidi na staili ya Zaiylissa, wakidai kuwa alionyesha ubunifu na mvuto wa kipekee uliomfanya kuwa mmoja wa nyota waliovutia zaidi usiku huo.
Licha ya maoni tofauti, jambo lililokuwa wazi ni kwamba Hamisa Mobetto na Zaiylissa walikuwa miongoni mwa watu walioteka hisia za wengi katika hafla hiyo, huku picha na video zao zikiendelea kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.
