Nature

Huyu Hapa Golikipa Mwenye Mafanikio zaidi Tanzania

NAIJATH ABASI IDRISA, Top Golie from JKT Queens! Usiku wa jana katoa mkwaju wa penati ambao ungewapa faida Gaborone United kuondoka na alama tatu dakika za mwishoni kabisa, ndiyo huyu Golikipa Bora wa Michuano ya CECAFA Women’s Champions League, Futsal 2025 iliyofanyika pale Morocco na Ngao ya Jamii ya Tanzania kwa Mwaka huu

Natamani watu waamke na kutazama kwa ukubwa mnoo soka la Wanawake namna linapiga hatua nchini, natamani sana siku moja huku watu wasaini Mabilioni kwaajili ya Uwekezaji wa klabu hizi za Wanawake na Ligi Kuu yao, natamani sana hizo nyakati zifike dada zetu waingize pesa nyingi sana kupitia mchezo huu pendwa kwa sasa Duniani

Kama haujamtazama NAIJATH ABASI IDRISA akiwa National Team ya Tanzania basi mtazame kwa sasa akiwa langoni kwenye mechi za Women’s CAF Champions League msimu huu pale nchini Misri, mtazameni vizuri akiwa na Jezi ya JKT Queens, One of the best Goalkeeper 💪🏽

Baada ya kutoka suluhu, 0-0 kwenye mchezo wa kwanza, mechi zijazo za JKT Queens ndani ya Kundi B ni dhidi ya Asec Mimosas jumatano pamoja na TP Mazembe siku ya jumamosi.

Let’s Goo!!.

Anaandika @officialevodiusoscar_

Related Posts