Jenerali Muhoozi wa Uganda Ampa Tano Rais Samia Kuwafurusha Wakenya
Jenerali Muhoozi Kainerugaba amempongeza Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akimtaja kuwa mmoja wa viongozi anaowapenda zaidi barani Afrika.
Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Muhoozi aliandika:
“Mama Suluhu Hassan anakuwa mmoja wa viongozi ninaowapenda zaidi Afrika. Hana masihara na ana maamuzi ya haraka! Asante sana Mama.”

Kauli hii imekuja kufuatia hatua ya Rais Samia kuvunja ukimya wake kuhusu kukamatwa na kuondolewa nchini kwa baadhi ya Wakenya mashuhuri waliokuwa nchini Tanzania mnamo Jumapili na Jumatatu wiki hii.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara Jumatatu, Mei 19, Rais Suluhu aliwalaumu wanaharakati wa Kenya kwa kile alichokitaja kuwa ni jaribio la kuvuruga amani ya Tanzania.
Alieleza kuwa baadhi ya wanaharakati hao walikuwa wakishindwa kuleta mabadiliko nchini mwao na sasa walikuwa wakijaribu kuingilia mambo ya Tanzania.
“Kama wamezuiliwa kwao, wasije kutuletea vurugu hapa,” alisema kwa msisitizo.
Rais Suluhu, ambaye ni kiongozi wa kwanza mwanamke kuongoza Tanzania tangu aapishwe Machi 19, 2021, alisisitiza kuwa taifa hilo lina kiwango cha juu cha utulivu wa kisiasa na haitavumilia yeyote anayejaribu kukitishia.
ALSO READ | Martha Karua wa Kenya Amjibu Rais wa Tanzania Kurudishwa Kenya