Jux Awakalisha Kina Wizkid, Burnaboy na Davido Nigeria, God Design Namba Moja
Msanii Jux ( @juma_jux ) kupitia wimbo wake “God Design”, aliomshirikisha nguli wa muziki kutoka Nigeria, Phyno amefanikiwa kuongoza chati za trending nchini humo ambapo Wimbo huo umewapita mastaa wakubwa kama Wizkid, Burna Boy, Davido na wengine jambo ambalo limewasha gumzo mitandaoni na kuibua pongezi kutoka kwa mashabiki wa pande zote mbili.
Kwa mara ya pili katika historia, Mtanzania mwingine ameweka rekodi kwa kuingiza video ya wimbo kwenye nafasi ya kwanza ya trending nchini Nigeria ambapo hii ni hatua kubwa inayodhihirisha ukuaji na ushawishi wa muziki wa Tanzania katika soko la Afrika Magharibi.
Jux sasa anaingia kwenye rekodi ya kuwa Mtanzania wa pili kufanikisha hili akifuata nyayo za Diamond Platnumz ambaye aliweka historia kupitia wimbo wa “My Baby”, aliouimba na Chike kutoka Nigeria na tukio hili linathibitisha kuwa muziki wa Bongo Flava unaendelea kuvuka mipaka na kushika chati kimataifa.