Klabu ya Simba SC wamekamilisha usajili na kumrejesha klabuni hapo Kiungo wa Kati Clatous Chota Chama ‘Tripple C’ kutoka klabu ya Singida Black Stars.
Chama anatarajiwa kuwa sehemu ya wachezaji 22 pamoja na benchi la ufundi ambao wataondoka kesho jumatano Januari 21, kuelekea nchini Tunisia kuwakabili Esperance katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
