
Lisasse Gueye Mchezaji Bora Ligi Kuu ya NBC Mwezi August 2026
Kiungo mshambuliaji wa Simba, Libasse Gueye, ametangazwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Agosti katika Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2026/27, baada ya kuonyesha kiwango bora na kuwa sehemu muhimu ya mafanikio ya timu yake.
Gueye alitoa mchango mkubwa katika michezo mitano ambayo Simba ilicheza mwezi huo, ambapo timu hiyo ilishinda michezo yote. Katika kipindi hicho, nyota huyo alifunga bao moja na kuhusika katika mabao mengine matano, jambo lililompa nafasi ya kuibuka mshindi wa tuzo hiyo.
Gueye aliwashinda Maxi Nzengeli wa Young Africans na Oscar Mwajanga wa Mbeya City, ambao walikuwa miongoni mwa wachezaji waliofika hatua ya mwisho ya mchakato wa Tuzo za Mwezi uliofanywa na Kamati ya Tuzo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
