Mamelodi Sundowns Yaanza Mazungumzo na Yanga SC Kumhuusu Beki Yao Kouassi

Klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini imeanza mazungumzo ya awali na Yanga SC kwa ajili ya kumsajili beki wa kulia raia wa Ivory Coast, Yao Kouassi Attohoula. Licha ya kuwa Sundowns bado haijawasilisha ofa rasmi mezani, miamba hiyo ya Afrika Kusini inasubiri ishara ya utayari kutoka kwa Yanga ili kuweka mezani dau kamili la usajili kuelekea dirisha dogo.

Taarifa zinaeleza kuwa Sundowns iko tayari hata kuaktisha mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 kwa kulipa ada ya uvunjaji wa mkataba endapo Yanga itaweka ngumu kuachana naye. Yao Kouassi anatajwa kuwa mmoja wa mabeki bora zaidi wa kulia waliowahi kucheza nchini, hatua inayoweka mtihani mkubwa kwa uongozi wa Yanga SC kuamua kumuuza au kumbakiza kikosini.

ALSO READ | Simba SC Yatinga Hatua ya Pili CAFCL Kwa Kishindo Baada ya Kuifumua Mighty Wanderers 6-1

Related Posts