TRATRA

Matokeo ya Usaili wa Mahojiano TRA

Kwa namna ya pekee Mamlaka ya Mapato Tanzania inamshukuru Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu
Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa KURIDHIA ombi la Mamlaka la kuongeza
nafasi za ajira 300 ambazo zilikasimiwa kwenye Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2025/26 kujazwa kwenye mchakato huu uliomalizika na hivyo kufanya idadi ya watakaoajiriwa kuwa 1,896 badala ya 1,596 ya awali.

Mtakumbuka kwamba Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilitangaza nafasi za kazi zipatazo 1,596
mwanzoni mwa mwezi wa Februari 2025, ambapo ilipokea jumla ya maombi ya kazi 135,027 kati yao 113,023 waliitwa kwenye usaili wa mchujo wa kuandika baada ya kukidhi vigezo na usaili huo uliofanyika tarehe 29 na 30 Machi, 2025. Wasailiwa waliofanikiwa kwenye usaili wa kuandika waliitwa kwenye usaili wa mahojiano uliofanyika tarehe 12 hadi 14 Mei, 2025, ambapo wasailiwa 6,325 walifanya usaili huo.

Mamlaka inapenda kuwataarifu waomba kazi wote walioshiriki kwenye usaili wa mahojiano kwamba matokeo ya usaili huo yatatolewa kesho tarehe 28/05/2025 kupitia barua pepe zao walizotumia kuombea kazi.

Wasailiwa 1,896 ambao wamefaulu na wameitwa kazini wanatakiwa kufika katika kumbi walizopangiwa tarehe 02 Juni, 2025 saa 1:00 asubuhi bila kukosa wakiwa na nyaraka muhimu kama zilivyoainishwa kwenye barua pepe zao.

Mamlaka inawashukuru waombaji wote walioonesha nia ya kufanya kazi na Mamlaka ya Mapato
Tanzania, na inawatakia kila la kheri katika ujenzi wa Taifa aidha, waombaji 4,429 ambao walishiriki usaili wa mahojiano na hawakufanikiwa kuitwa kazini, taarifa zao zitahifadhiwa kwenye kanzidata ya Mamlaka kwa matumizi ya baadaye.

Kwa taarifa zaidi, wasiliana na Mamlaka kwa kutumia mawasiliano yafuatayo;-
Tovuti: www.tra.go.tz
Namba za simu bila malipo:
0800 780078 au 0800750075 au 0800110016
WhatsApp: 0744 23 33 33
Barua pepe: [email protected] au [email protected]

‘‘Pamoja Tunajenga Taifa Letu’’
Imetolewa na;
MOSHI JONATHAN KABENGWE
KWA NIABA YA KAMISHNA MKU

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *