Taarifa zinaeleza kuwa Ndugu George Mayawa, aliyekuwa Mjumbe wa Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi (Kamati ya Masaa 72), amejiuzulu nafasi hiyo kwa kile kinachodaiwa kuwa ni sababu binafsi.
Akithibitisha taarifa hizo, Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Steven Mguto amesema:
“Kweli George ameniandikia barua ya kujiuzulu ila mara nyingi huwa anakosa vikao maana ana kazi nyingi… George kwenye barua yake amesema amebanwa na kazi nyingi ila sio kama inavyosemwa.”
Hata hivyo, kujiuzulu kwake kumekuja wakati ambapo Kamati hiyo iko chini ya presha mkubwa kutokana na masuala ya uendeshaji wa ligi.