MSIGWA: Serikali haiwezi kumuwekea SUMU mtu yeyote, kuhusu TUNDU LISSU ni uongo

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekanusha vikali madai ya kuwepo kwa njama ya kumtilia sumu kiongozi wa chama cha upinzani CHADEMA, Tundu Antipas Lissu, ambaye kwa sasa yuko rumande akisubiri uamuzi wa mashauri yake mahakamani.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, Julai 3, 2025 Serikali imezitaja taarifa zinazosambazwa juu ya madai hayo kuwa ni “za uzushi, na zisizo na msingi wowote, na zenye lengo ovu la kuchafua sifa ya Tanzania kitaifa na kimataifa.”

“Serikali inawaomba wananchi kupuuza taarifa hizo kwa kuwa hazina ukweli wowote. Tundu Antipas Lissu, anayetajwa na wanasiasa hao wa nje ya nchi, pamoja na taarifa kwa umma ya chama chake cha siasa, anakabiliwa na mashtaka Mahakamani kwa mujibu wa Sheria na anashikiliwa gerezani mpaka hapo shauri lake litakapohitimishwa na Mahakama”, ameeleza Msigwa.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa Serikali haijawahi kuwa na mpango wa kumdhuru mtu yeyote aliyeko kizuizini na kwamba taarifa hizo ni sehemu ya kampeni ovu ya kuchafua sifa ya Tanzania kimataifa.

Lakini kabla ya taarifa hiyo ya serikali, Chama cha CHADEMA kilikuwa kimetoa taarifa rasmi tarehe 2 Julai 2025 kikieleza wasiwasi wake kuhusu usalama wa mwenyekiti wake Tundu Lissu. Kupitia kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi, Brenda Rupia, CHADEMA kilisema:

“Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinapenda kuujulisha umma kuwa kimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa zinazodai kuwa Mhe. Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, kuna mipango ya kuwekewa sumu akiwa kizuizini”.

Taarifa hiyo ya CHADEMA pia ilinukuu kauli ya David McAllister, Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Ulaya (European Parliament), aliyeeleza wasiwasi wake kuhusu usalama wa Tundu Lissu kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X (zamani Twitter).

“Nina wasiwasi mkubwa kuhusu ripoti za kutisha za jaribio la kumtilia sumu kiongozi wa upinzani wa Tanzania Tundu Lissu akiwa kizuizini.”

Kwa mujibu wa CHADEMA, wanataka uchunguzi huru ufanyike na pia Serikali iwajibike kuhakikisha usalama wa Lissu akiwa rumande, huku wakitoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kufuatilia kwa karibu suala hilo.


Alikataa kuolewa ili amkomboe mama yake... Lakini mama ndiye aliyemuuza!

GORYANAH –Hii ni story ya Moto Sana yenye hisia na Mafunzo, binti jasiri anayepambana na siri nzito, umaskini na hatari kubwa kwa ndoto zake! Pakua app yetu ufurahie Sehemu ya 1 Hadi ya 5,na mwendelezo wake kila JUMAMOSI SAA MOJA KAMILI JIONI BURE!

BONYEZA HAPA KU DOWNLOAD.

Ukiona ujumbe wa allow notification bonyeza allow ili uwe mwanafamilia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *