Msukuma awaonya matajiri wa Katoro wanaorusha fedha

Msukuma awaonya matajiri wa Katoro wanaorusha fedha
Msukuma awaonya matajiri wa Katoro wanaorusha fedha

Msukuma awaonya matajiri wa Katoro wanaorusha fedha

Wakati wachimbaji wa Dhahabu na matajiri wa madini wa Katoro mkoani Geita wakizidi kujizolea umaarufu na sifa kutokana na utamaduni wao wa kumwaga na kutunza fedha na kuandaa sherehe za kufuru, tahadhari imetolewa dhidi yao.

Tahadhari hiyo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Kasheku ‘Msukuma’, leo mkoani Mwanza wakati akizungumza katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa Jumuiya ya Wanajiolojia Tanzania (TGS).

Msukuma ambaye pia ni Mjumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya nishati na madini, amesema jambo hilo siyo zuri na linaonyesha wachimbaji hao hawana uelewa, hivyo wanahitaji msaada wa wataalam wawasaidie ili wawe na mwisho usio na aibu.

Amesema ana uzoefu wa muda mrefu na fedha zinazotokana na madini kwani amekuwa mchimbaji tangu miaka ya 1980, hivyo ameshuhudia watu wengi wa aina hiyo ambao kwa mujibu wake waliishia pabaya na kwa aibu.

Amesema yanayotokea Katoro siyo dhambi bali inaoonyesha watu hawakuwa wamejiandaa baada ya kupata fedha nyingi baada ya muda mrefu wa kusota.

“Kwa sababu baada ya kutupa huna asset (mali) huna kila kitu ukirudi duarani (shimoni) unakuta hamna dhahabu, sasa haya yanayotokea Katoro si dhambi kwa sababu pia tulikaa muda mrefu bila kupata hela lakini sasa wamezipata hela hatujajiandaa na matumizi,” amesema Msukuma.

Related Posts