Kulingana na taarifa iliyotolewa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kupitia kwenye Mitandao yake ya Kijamii, Naibu Katibu Mkuu Bara Mhe. Amani Golugwa ametoka kwa dhamana usiku huu huku wanachama wengine wakiachiwa na kutakiwa kuripoti kesho.
Mapema leo Polisi ya Dar Es salaam ilibainisha kuwa Imearifiwa kuwa, kukamatwa kwa kiongozi huyo wa juu wa chama cha upinzani kulitokana na “taarifa za siri kuwa amekuwa na mienendo ya kuondoka na kurudi Nchini bila kufuata taratibu za kisheria hapa Nchini.”
Kwasasa, kulingana na Polisi uchunguzi wa kina unaendelea ukishirikisha Vyombo vingine vya Usalama, huku Polisi wakiahidi kutoa taarifa zaidi kadri hatua zitakavyopigwa.