Nandy ametangaza kupoteza pete zake za ndoa. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Nandy amewaomba mashabiki na wananchi kwa ujumla kusaidia kuipata pete hizi za thamani .
Kupitia ujumbe wake, Nandy amesema atatoa zawadi ya shilingi milioni 10 kwa mtu atakayesaidia kuipata pete hiyo au kutoa taarifa muhimu ikiwa pete hiyo imefikishwa kwa sonara. “Pete zangu zina memory kubwa sana maishani mwangu,” ameandika Nandy, akionyesha wazi jinsi pete hizo zilvyokuwa za muhimu kwake.
Swali: Unaweza kumrudishia Nandy pete zake za ndoa ili upate milioni 10?