Pep Guardiola Afunguka ” Kuwapokonya Senagal Kombe Kutaathiri Taswira na Uaminifu wa Soka”

Pep Guardiola Afunguka " Kuwapokonya Senagal Kombe Kutaathiri Taswira na Uaminifu wa Soka"
Pep Guardiola Afunguka ” Kuwapokonya Senagal Kombe Kutaathiri Taswira na Uaminifu wa Soka”

Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola, ameanzisha mjadala kimataifa baada ya kuhoji uamuzi wa CAF kubadili matokeo ya fainali ya AFCON 2025 na kuipa Morocco ubingwa.

Guardiola amesema hakujapatiwa maelezo ya kina kuhusu msingi wa uamuzi huo, akisisitiza kuwa kubadilisha mshindi wa mashindano makubwa bila uwazi kunaweza kuathiri taswira na uaminifu wa soka duniani. Ameongeza kuwa maamuzi kama hayo yanahitaji ushahidi wa kutosha na mawasiliano rasmi ili kulinda heshima ya mchezo.

Kauli hiyo imekuja wakati mjadala mkali ukiendelea Afrika na kimataifa, huku wadau wakitaka CAF kutoa ufafanuzi zaidi. Wakati huohuo, presha inaendelea kuongezeka kwa CAF huku wengi wakisubiri uamuzi wa mwisho kutoka Court of Arbitration for Sport,(CAS) ambao unaweza kuwa na athari kubwa kwa uendeshaji wa mashindano ya soka barani Afrika.

 

Related Posts